Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554320

Habari za michezo of Monday, 30 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco

Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco

KIKOSI cha Yanga leo kimepoteza katika mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.Alianza  Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.