Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 559090

Soccer News of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga Yaipiga bao Simba Mauzo ya Tiketi 2020/2021

Orodha ya Vilabu 20 na mauzo yao ya tiketi msimu wa 2020/2021 Orodha ya Vilabu 20 na mauzo yao ya tiketi msimu wa 2020/2021

Viingilio katika mechi za Ligi kuu Tanzania Bara ni Moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ambavyo Vilabu hufaidika navyo.

Japokuwa mara kwa mara suala la Mauzo ya tiketi katika michezo ya Ligi kuu bara limekuwa na changamoto kwa mashabiki na wapenda soka, Lakini Bodi ya Ligi (TPLB) imekuwa ikijitahidi kushughulika nazo kwa kuona eneo hilo halipaswi kuwa na mashaka.

Bodi ya Ligi, Leo Septemba 22, imetoa orodha ya timu 20 zilizoongoza kwa makusanyo ya viingilio milangoni na katika Orodha hiyo klabu ya Yanga imeonekana kuongoza huku aliekuwa bingwa wa Ligi kuu msimu uliopita, Simba SC wakikamata nafasi ya pili.