Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 11Article 562609

Soccer News of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga hawataki kujadili sakata la nembo ya Mdhamini

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli

Yanga haina muda na rangi nyekundu ya Twiga katika nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu Benki ya NBC.

Hilo limejidhihirisha kutokana na maneno ya Afisa Habari wa Yanga ,Hassan Bumbuli alipoulizwa swali iwapo watavaa jezi zenye nembo hiyo kama ilivyo kwani walishawahi kugomea nembo ya mdhamini miaka ya nyuma.

"Hicho ndicho kitu ambacho mnakijua waandishi wa nchi hii, badala tuongelee vitu vya maendeleo ya mpira mnaongelea vitu visivyo na msingi"

"Klabu ya Yanga inajulikana na taratibu zake zinajulikana, utamaduni wa Yanga upo wazi kabisa"

"Kumekuwa na maneno mengi yanayosambaa kuwatia hofu mashabiki, wananchama na wapenzi wa Yanga, sisi hilo hatushughuliki nalo na tunawataka wapenzi wetu wasiwe na wasi wasi" amesema Bumbuli

Kumezuka minong'ono katika mitandao ya kijamii kuwa picha ya Twiga katika nembo ya NBC ina alama nyekundu huku klabu ya Yanga ikiwa ni miongoni mwa timu inayoshiriki ligi kuu na ni mwiko kwake kuvaa rangi nyekundu katika jezi zake.

Majibu ya yote haya ni kuupa muda nafasi tunaweza kujua kama kweli Yanga wanaweza kubadili kanuni za mamlaka za Soka ama la.