Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 02Article 560980

Soccer News of Saturday, 2 October 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga hii unagusa unaachia

Pira biriani lilipigwa kwa Mkapa Pira biriani lilipigwa kwa Mkapa

Mashabiki wa klabu ya Yanga wamejikuta muda wote wakiwa na furaha uwanjani kutokana na kikosi chao kucheza pasi zilizokuwa zinawapa burudani uwanjani hapa.

Wachezaji wa Yanga walikuwa wanacheza mchezo wa kugusa mpira mara mbili hali iliyowafanya mabeki na viungo wa Geita wawe na wakati mgumu kuwazuia.

Mabeki wa  kati Yanga, Dickson Job na Yanick Bangala walikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanacheza aina ya soka hilo la kuvutia.

Upande wa viungo napo Mukoko na Feisal nao walikuwa wanacheza aina hiyo ya soka lakini kiungo wa Geita Gold, Maka Edward alikuwa anatumia umbo lake kuwapa wakati mgumu.

Upande wa ushambuliaji Yanga, Fiston Mayele yeye alikuwa anacheza pia kama wenzake kakini Yacouba Sogne alikuwa anakaa sana na mpira.

GEITA WAMO Licha ya kwamba walikuwa nyuma kwa bao moja kikosi cha Geita kilichokuwa kinanolewa na kocha Etiene Ndayiragije waliendelea kucheza soka safi.

Utulivu wa kihesabu za beki Oscar Masai kwa Fiston Mayele zilimfanya mshambuliaji huyo muda wote awe chini ya ulinzi.

Washambuliaji wa Geita, Lyanga na Mahadhi walikosa utulivu licha ya kuwa wanawapa changamoto mabeki wa Yanga.