Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 26Article 544372

Habari za michezo of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Yanga kufanya Mkutano Mkuu kesho, Ajenda 12 mezani

Msola, Mwenyekiti wa Yanga Msola, Mwenyekiti wa Yanga

Klabu ya Yanga ya Dar es salaam itafanya mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo kesho Juni 27, 2021. Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa DYCCC, Chang'ombe mkabala na Chuo cha DUCE karibu na uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

Submitted by Ibra Kasuga on Jumamosi , 26th Jun , 2021 Mwenyekiti wa Yanga Dkt. Mshindo Msolla

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dkt. Mbete Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo wameziweka wazi ajenda 12 za mkutano huo, wamefanya hivyo ikiwa ni kwa mujibu wa Ibara 20 (2) ya Katiba ya Yanga.

Ajenda mojawapo itakuwa ni kuhusu Kupitia mapendekezo ya marekebisho ya Katiba kuelekea kwenye mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Hizi hapo Ajenda zote za Mkutano Mkuu wa Yanga

 

1. Uhakiki wa wajumbe wanaohudhuria mkutano

2. Kuthibitisha ajenda za mkutano

3. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita

4. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita

5. Hotuba ya Mwenyekiti wa Klabu

6. Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji

7. Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia

8. Kuthibitisha taarifa za chombo cha ukaguzi na hatua zilizochukuliwa na vyombo vya utendaji

9. Kuthibitisha Bajeti kwa mwaka unaofuata

10. Uchaguzi wa nafasi zilizo wazi

11. Kupitia mapendekezo ya marekebisho ya Katiba na taratibu za Yanga

12. Majadiliano ya mapendekezo yaliyowasilishwa na wajumbe au Kamati ya Utendaji.