Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553573

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga kutambulisha jezi za msimu mpya leo

Mkurugenzi wa uwekezaji Injinia Hersi Said (aliesimama) na Viongozi wa Yanga Mkurugenzi wa uwekezaji Injinia Hersi Said (aliesimama) na Viongozi wa Yanga

Klabu ya Dar es Salaam Young Africans leo hii wanaenda kutambulisha jezi zao mpya kwa msimu mpya wa 2021/2022.

Yanga wanaenda kutambulisha jezi watakazotumia nyumbani msimu ujao, ugenini pamoja na jezi ya ziada.

Tukio hilo linatarajiwa kufanyika leo Agosti 25, katika ukumbi wa Mlimani City na pia Mashabiki watapata nafasi ya kununua jezi huku wakielekea katika kilele cha wiki ya mwananchi Jumapili ya wiki hii.

Yanga katika shughuli hiyo itaambatana na Afisa Habari mpya wa klabu hiyo, Haji Manara katika kunogesha tukio hilo.