Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 26Article 574135

Soccer News of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Yanga kwafukuta, Makocha hawaelewani, Nabi afikiria kusepa

Makocha wa Yanga, Kaze na Nabi Makocha wa Yanga, Kaze na Nabi

Kuna taarifa zinazoeleza kuwa hakuna maelewano ya kikazi baina ya makocha wawili Nasreddin Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze ndani ya kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga.

Inasemekana kuwa Kaze amekuwa akiingilia majukumu ya kocha Mkuu katika vitu mbalimbali na hivi karibuni katika pambano dhidi ya Namungo FC kule Ilulu Lindi, Kaze aliwahi vyumbani muda wa mapumziko na kuanza kutoa maelekezo kabla ya Nabi.

Hali hiyo haipendezwi na Nabi na imeanza kumshinda na inatajwa huenda akaondoka kikosini humo.

Hata hivyo alipotafutwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Senzo Mazingisa alisema hizo ni fununu na hana muda wa kuzijibu, anachokiamini ndani ya Yanga hali ni shwari.

Senzo amesema hizo ni njama za kuwatoa katika maandalizi yao kueleka mechi yao dhidi ya Mbeya Kwanza.

Yanga itacheza wake unaofuata wa Ligi Kuu ugenini dhidi ya Mbeya Kwanzaa Novemba 30.