Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560386

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga ndio kwanza kumekucha Ligi kuu Bara

Beki wa Kagera Sugar akijaribu kumzuia Fiston Mayele Beki wa Kagera Sugar akijaribu kumzuia Fiston Mayele

Mabingwa wa Kihistoria, Klabu ya Dar Young Africans, Timu ya Wananchi, ni kweli wana jambo lao msimu huu, na ni kweli wanakitaka kila kikombe msimu huu.

Katika mchezo wao hii leo dhidi ya Klabu ya Kagera Sugar, kule katika dimba la Kaitaba wamefanikiwa kuondoka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 na kuacha burudani ya kutosha kwa Mashabiki wao.

Goli pekee la Yanga katika mchezo huo limewekwa wavuni na kiungo Kipenzi cha mashabiki wa Timu hiyo Feisal Salum "Fei toto" dakika ya 24 ya mchezo.

Lakini kivutio kikubwa katika mechi hiyo ni viango vinavyoonyeshwa na wachezaji wapya waliosajiliwa na kikosi cha Yanga namna wanavyotakata.

Ktika mechi dhidi ya Kagera bado Kiungo mganda Khalid aucho ameendellea kukonga sana nyoyo za mashabiki wa wanajangwani bila kumsahau kiungo wa ulinzi Yannick Bangala.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kule karatu Polisi tanzania imetakata na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya watoza ushuru wa Manispaa ya Kinondoni KMC.

Magoli ya Polisi Tanzania yamefungwa na Vitalis Mayanga 3' na 20'.