Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 13Article 557245

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga ni mwendo wa hamasa mpaka kieleweke

Straika wa Yanga, Heritier Makambo Straika wa Yanga, Heritier Makambo

Baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, kwa Mkapa Jijini Dare es Salaam na kuleta taharuki kubwa kwa Mashabiki wake.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umekuja na mipango madhubuti kuhakikisha wanatoboa Septemba 19 katika mechi ya marudiano dhidi ya Rivers United kule Naijeria.

Mchezo wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kwa kuwa kila timu inasaka ushindi, ili iweze kusonga hatua inayofata japokua Yanga wana mlima mrefu wa kuupanda.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa wananafasi ya kuibuka washindi kama Rivers waliweza kushinda Ugenini hali kadhalika hata wao pia wana nafasi hiyo.

Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Klabu ya Yanga, kuna Jumbe mbali mbali za kuhamsisha kuelekea mchezo huo wa marudiano Septemba 19. Jumbe hizo ni pamoja na;

"Mapambano yanaendelea" "Tutarudi tukiwa imara zaidi"

Je, ni kweli Yanga watafanikisha azma yao, bila shaka muda ndio msema kweli, tusubiri hiyo siku ya mchezo