Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554290

Habari za michezo of Monday, 30 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga waendeleza utamaduni wa suti

Yanga waendeleza utamaduni wa suti Yanga waendeleza utamaduni wa suti

WACHEZAJI na Viongozi wa benchi la Ufundi la Yanga, leo katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi wameingia uwanjani Benjamin Mkapa wakiwa wote wamevalia suti za rangi ya kijivu, mashati meupe na raba nyeupe.

Waachezaji na Viongozi hao waliingia uwanjani hapo wakionekana kupendeza na wenye furaha kisha kuanza kuzunguka uwanja wakiwasalimu Mashabiki zao.

Wakati wakizunguka uwanjani hapo, msherejeshaji Dakota Dalavida alikuwa akizunguka nao hatua kwa hatua huku akiita ‘Wananchiiiii’ na ‘Sisi tuna..’ na Mashabiki kuitikia “Tuna Watu”.

Tukio hilo liliwafanya karibu mashabiki wote waliokuwepo uwanjani hapo kunyanyuka kwenye viti vyao na kuamsha bonge la shangwe.

Baada ya kumaliza kuzunguka Uwanja kusalimia mashabiki wao waliingia uwanjani na kupata picha ya pamoja huku wakiimba wimbo wa Yanga laivu wakiongozwa na kipa Ramadhan Kabwili.

Baada ya hapo waliendelea na taratibu nyingine kisha kurejea katika vyumba vya kubadili nguo kujiandaa na mtanange wa kirafiki dhidi ya Zanaco kutoka Zambia.