Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 27Article 540139

Habari za michezo of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Yanga waipania Biashara

Yanga waipania Biashara Yanga waipania Biashara

SIKU moja baada ya kikosi cha Yanga kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasredden Nabi amesema kazi kubwa iliyopo mbele yake kwa sasa ni kuwaanda vijana wake kwa ajili ya kuwamaliza wapinzani wao Biashara United na kutinga fainali.

Yanga ambayo ndio mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo itacheza na Biashara United ya Mara katika hatua ya nusu fainali itakayopigwa kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora mwezi ujao.

Akizungumza na HabariLEO jana, Nabi alisema anachokifanya kwa sasa ni kuwafuatilia wapinzani wao ili kujua ubora walionao na udhaifu wao, lengo likiwa ni kujua mbinu mbadala za kutumia ili kuwamaliza watakapokutana nao.

“Nafahamu kuwa wapinzani wetu wana kocha mpya, kwa hiyo inabidi kuangalia mechi yao waliyocheza na Namungo FC na mechi nyingine za ligi ambazo walikuwa chini yake na baada ya hapo nitajua nitumie mfumo gani ambao utakwenda kutupa ushindi na kutinga fainali ya FA,” alisema Nabi.

Kocha huyo raia wa Tunisia alisema anajua hautakuwa mchezo rahisi kwa timu zote mbili, lakini amepania kuweka rekodi akiwa na vijana hao wa Jangwani kwa kutwaa ubingwa wa taji hilo licha ya muda mchache aliokuwa nao tangu akabidhiwe timu hiyo.

Alisema amekuwa akizungumza na wachezaji wake kila baada ya mazoezi akiwataka kuongeza umakini na juhudi katika kila mechi ya mashindano yote wanayoshiriki ili kurudisha heshima ya timu hiyo na wao wenyewe binafsi.

Kocha huyo alisema amefuraishwa na namna kikosi chake kilivyocheza mechi ya robo fainali dhidi ya Mwadui FC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yote yakifungwa na kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke.

Join our Newsletter