Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 551968

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga yaanza tizi Morocco

Kiungo wa Yanga,Feisal Salum akiwa uwanja wa Mazoezi Kiungo wa Yanga,Feisal Salum akiwa uwanja wa Mazoezi

Klabu ya Wananchi Yanga, leo wameanza mazoezi rasmi huko nchini Morocco ambako ndipo walipoweka kambi wakijiandaa na Msimu mpya 2021/2022.

Yanga iliondoka nchini Jumapili Agosti 15 mchana na leo ndio nsiku ya kwanza wameingia katika uwanja wa mazoezi wakijiandaa na mechi za ligi na kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wachezaji wanaonekana kufurahishwa na hali ya hewa ya morocco na wote wanaonekana kuwa fiti na wamejipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa upande wa michuano ya Vilabu barani Afrika Yanga itaanza kukipiga na klabu ya Rivers united kutokea kule nchini Nigeria.