Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 16Article 551683

Habari za michezo of Monday, 16 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Yanga yafuata makali Morocco

Yanga yafuata makali Morocco Yanga yafuata makali Morocco

MSAFARA wa Klabu ya Yanga umeondoka nchini jana, kuelekea Morocco kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 11 kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga watapitia Dubai na kisha kutua Morocco katika jiji la Casablanca ambako ndipo watakapo weka kambi yao.

Kocha Razak Siwa, ambaye ameongozana na wachezaji amesema kambi hiyo itawasaidia kukiimarisha kikosi chao kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Alisema anafurahi kuona wachezaji wote wapo kwahiyo maandalizi yao yatafanyika kikamilifu lengo kubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano yote.

Kwaupande wake Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe, alisema kambi hiyo inatoa nafasi nzuri kwa benchi la ufundi na wachezaji kujipanga vizuri kabla ya msimu mpya kuanza.

“Hongera kwa uongozi wetu kufanikisha kambi hii ambayo itawasaidia wachezaji na sisi benchi la ufundi kujiandaa na kuweka malengo yetu sawa katika msimu mpya tunaoelekea kuuanza mwezi ujao, wachezaji wote wapya na wazamani wote tupo safarini kwa ajili ya kambi hiyo,” alisema Hafidhi.

Timu hiyo imeondoka na kikosi cha wachezaji 28 na viongozi 16 wa benchi la ufundi wachezaji walioondoka ni Makipa Djigui Diarra, Erick Johora na Ramadhani Kabwili.

Mabeki wa pembeni ni Djuma Shabani, Kibwana Shomari, David Brayson, Yassin Mustapha, Adeyum Saleh, Paul Godfrey, mabeki wa kati ni Yannick Bangala, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto. Viungo wa kati ni Khalid Aucho, Zawadi Mauya, Mukoko Tomombe, Saido Ntibazonkiza, Feisal Salum na Balama Mapinduzi

Viungo wa pembeni ni Jesus Moloko, Farid Mussa, Deus Kaseke, Dickson Ambundo na Ditram Nchimbi. Washambuliaji yupo Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yaccouba Sogne na Yusuph Athumani

Yanga itaanza kuchanga karata zake kwenye mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwakati ya Septemba 10-12 dhidi ya Rivers United ya Nigeria.