Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 552052

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Yanga yaifanyia u-mafia TP-Mazembe

Yannick Bangala Litombo, beki mpya wa Yanga Yannick Bangala Litombo, beki mpya wa Yanga

Yanga wanatarajiwa kumtambulisha beki wao mpya, Mkongomani, Yannick Bangala Litombo aliyekuwa anaichezea RS Berkane ya nchini Morocco.

Inaelezwa kuwa, usajili huo umekuja baada ya Yanga kuwapiga bao TP Mazembe ya DR Congo ambayo nayo ilikuwa ikiifukuzia saini ya beki huyo.

Mwandishi na mtangazaji wa michezo kutoka Lubumbashi, DR Congo, Elisha Elagi, alisema: “Litombo ni beki haswa, kwa sababu amecheza timu ya taifa kwa muda mrefu sana na alikuwa aende Mazembe, nafikiri Yanga wamewazidi ujanja, hakika atakwenda kuwasaidia.”Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Thabit Kandoro, amesema kuwa:

“Kwa sasa Yanga tukimtaka mchezaji yeyote hatuwezi kumkosa, hii ni timu kubwa.”Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, amesema, kuwa usajili walioubakisha kwa sasa ni wa Litombo ambaye atatambulishwa leo mara bada ya kujiunga na wachezaji wenzake kambini nchini Morocco.

Said amesema, usajili wa Litombo umeshakamilika kwa kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili, huku akisubiri kusaini mkataba wa kudumu leo Jumanne baada ya kujiunga na kambi.

“Litombo tutamkuta hukohuko Morocco mara baada ya kuvunja mkataba na timu yake ya Berkane ya nchini huko.“Tuliona kama tunamsumbua Litombo kumleta Tanzania na kumrudisha huko Morocco, hivyo tulimwambia atusibirie huko baada ya kusaini atatambulishwa na kujiunga na timu,” amesema Said.