Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559864

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga yaifuata Kagera Sugar bila mastaa wake wanne

Yanga yaifuata Kagera Sugar bila mastaa wake wanne Yanga yaifuata Kagera Sugar bila mastaa wake wanne

KIKOSI cha nyota 23 wa Yanga kimeondoka leo kuelekea Bukoba tayari kwa mchezo wao wa kwanza wa Ligi dhidi ya Kagera Sugar Jumatano.

Yanga inatarajia kuwakosa nyota wake wanne kwenye mchezo huo ambao wamebaki Dar es Salaam, Yassin Mustafa, Balama Mapinduzi, Saido Ntibazonkiza, Mukoko Tonombe na Dickson Ambundo.

Nyota hao 23 wameongozwa na benchi zima la ufundi likiwa na kocha mkuu Nesreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh alisema wachezaji wote waliosafiri nao wapo kwenye hari nzuri na wamejiandaa kwaajili ya ushindi kwenye mchezo huo.

“Wachezaji waliobaki watatu hawapo fiti wataungana natimu kwenye mchezo unaofuata na Mukoko anaendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu, wote tunaosafiri nao sasa wanahari ya mchezo na wameahidi ushindi,” alisema.

Nyota walioondoka ni makipa Djigui Diarra,Erick Johola, Ramadhan Kabwili, mabeki Djuma Shaban, Kibwana Shomari, David Bryson, Adeyum Saleh, Abdallah Shaibu, Dickson Job Bakari Nondo na Yanick Bangala.

Viungo Khalid Aucho, Deus Kaseke, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Jesus Moloko Ditraim Nchimbi na washambuliaji ni Fiston Mayele, Yusuph Athuman, Yacouba Sogne na Heritier Makambo.