Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585310

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Yanga yamkana Chama “Hatukuwa na nia ya kumsajili”

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli

Klabu ya Yanga imesema kutokana na kuwa vizuri kifedha hakuna hata mchezaji mmoja ambaye anaweza kuruka kwenye usajili pale tu wakionyesha nia ya kumsajili kutokana na ubora wake.

Kauli ya Yanga inakuja baada ya kuwepo kwa maneno kuwa wameshindwa kumshawishi kifedha kiungo mshambuliaji wa RS Berkane Clatous Chota Chama na mchezaji huyo kuhusishwa kujiunga na miamba ya soka Msimbazi, klabu ya Simba.

Akijibu kauli hiyo wakati akizungumza na Wasafi FM, Afisa Habari wa Timu ya Wananchi Yanga Hassan Bumbuli amesema hakuna mchezaji ambaye anaweza kuhitajika na Yanga kwa sasa kisha wakashindwa kumsajili.

“Kwa sasa tuko vizuri. Hakuna mchezaji ambaye tunaweza kumhitaji tukashindwa kumpata. Chama hatukumhitaji bali Chama alihitajika na Waandishi wa Habari kumuona anacheza Yanga. Sisi hatukumhitaji hivyo”, alisema Bumbuli.

Kwa sasa Simba inaongoza mbio za kuwania saini ya Chama ambapo baadhi ya tetesi zinaeleza kuwa Wekundu wa Msimbazi wameshakamilisha uhamisho wa kiungo huyo kwa mara ya pili baada ya kuitumikia Simba awali.