Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 20Article 558436

Habari za michezo of Monday, 20 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Yanga yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika

Yanga yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga yaondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika

Yanga imeaga rasmi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupoteza mchezo wa leo kwa bao 1-0 na hivyo kupoteza jumla ya mabao 2-0 baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa wiki moja iliyopita kupoteza pia.

Mabingwa hao wa kihistoria itabidi wasubiri mpaka msimu ujao ili kushiriki tena michuano hiyo.

Awali kabla ya mchezo wa leo, msemaji wa timu hiyo,Haji Manara alisema walifanyiwa baadhi ya vigisu hali iliyopelekea kugomea mchezo huo na kwamba kama kusingekuwa na haki wasingecheza.

Manara alisema wachezaji wao walipimwa virusi vya corona cha kushangaza saa moja kabla ya mchezo huo majibu hayakutoka, hata hivyo walipopokea majibu hayo waliambiwa kuwa nyota wao, Feisal Salum, Mukoko Tonombe na Yacouba wana covid-19.

Kwenye video fupi iliyochapishwa na Yanga kwenye mtandao wa Instagram, Manara alisikika akisema “Kama haki haitatendeka mechi hii hatuchezi kama wamekuja na mbinu zao za kihuni hatuchezi.”

Hata hivyo baada ya muda mfupi walionekana wachezaji hao kwenye kikosi cha kwanza kilichoanza mchezo huo na wote waliche