Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553060

Soccer News of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga yasitisha kambi yake Morocco, Kurejea kesho mchana

Kikosi cha Yanga kilichokua kimeweka kambi nchini Morocco, sasa kinarejea nchini Kikosi cha Yanga kilichokua kimeweka kambi nchini Morocco, sasa kinarejea nchini

Timu ya Wananchi Yanga imesitisha kambi yao ya maandalizi ya Msimu ujao iliyokua huko marrakech nchini Morocco, na wanarejea nchini kwa ajili ya kumalizia maandalizi hayo.

Maamuzi hayo yametangazwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM mhandisi Hersi Said akisema zipo sababu mbalimbali zilizowapelekea kufanya maamuzi hayo.

Hersi amesema kumeguka kwa baadhi ya wachezaji wao ambao wanatakiwa kujiunga na timu za taifa ndio sababu ya kwanza ambapo jumla ya wachezaji wao nane kuitwa timu za taifa.

"Ukiangalia tumeona timu itameguka hivi karibuni wachezaji wetu wasiopungua nane wanatakiwa kwenda kujiunga na timu za taifa utaona hapo tutabaki na wachezaji wachache sana hapa,"amesema Hersi

"Vile vile kuna changamoto ya kiusafiri hivyo tumeonelea ni heri turudi nyumbani tumalizie kambi yetu na tuhitimishe Tamasha la wiki ya Mwananchi" ameongeza Injinia Hersi

Baadhi ya wachezaji wa Yanga walioitwa timu zao za Taifa ni pamoja na Khalid Aucho,golikipa wa Mali,Diarra, Mukoko Tonombe na wengine wengi.

kwa mujibu wa Hersi timu itaondoka kwa awamu mbili, huku kundi la kwanza likiondoka leo kupitia Dubai na watawasili nchini kesho majira ya saa saba mchana na Shirika la ndege la Fly Emirates.