Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 27Article 544486

Habari za michezo of Sunday, 27 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga yatenga bajeti ya Sh7.9 bilioni 2021/22

Yanga yatenga bajeti ya Sh7.9 bilioni 2021/22 Yanga yatenga bajeti ya Sh7.9 bilioni 2021/22

Klabu ya Yanga imetenga bajeti ya Sh7, 984, 406, 422 msimu wa 2021/2022.

Bajeti hiyo imetolewa kwa wanachama kwenye mkutano mkuu unaoendelea kwenye ukumbi wa DYCC, Dar es Salaam.

Katika bajeti hiyo, klabu ya Yanga imeanisha kukusanya Sh8, 149, 000, 000 kutoka kwenye udhamini, jezi, match day, social media na ada za uanachama.

Katika udhamini, Yanga imeanisha kukusanya Sh4, 901,736,274 wakati kwenye mapato ya jezi itakusanya Sh350 milioni.

Ada za wanachama klabu hiyo itakusanya Sh 2,040,000,000, match day Sh565 Milioni na kwenye social media Sh960 milioni.