Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559963

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga yatua Kagera, mapokezi yake usipime

Msafara wa Kikosi cha Yanga baada ya Kuwasili Mkoani Kagera Msafara wa Kikosi cha Yanga baada ya Kuwasili Mkoani Kagera

Kikosi cha Wanajangwani, Young Africans kimewasili salama Mkoani Kagera ,tayari kuwavaa wenyeji Kagera Sugar, Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara.

Yanga itatupa karata yake ya kwanza msimu huu wa Ligi 2021/2022 siku ya Jumatano dhidi ya Kagera katika uwanja wa Kaitaba.

Yanga imepokelewa kwa Shangwe kubwa sana na Mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo na kusindikizwa mpaka Hotelini wanapokwenda kufikia.