Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 16Article 551794

Soccer News of Monday, 16 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga yatua Morocco, Aucho kesho

Kikosi cha Wachezaji wa Yanga Kikosi cha Wachezaji wa Yanga

Msafara wa kikosi cha Yanga umewasili jijini Casablanca tayari kwa maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi.

Yanga imetumia saa 12 angani wakisafiri safari ya masaa matano kutoka Dar es Salaam mpaka Dubai kisha kisafiri tena saa 7 kutoka Dubai mpaka jijini Casablanca wakitua Uwanja wa Mfalme Mohamed 5.

Yanga imewasili jijini Casablanca leo mchana na kundi la wachezaji 21 waliotokea jijini Dar es Salaam kupitia Dubai huku wengine wakitangulia na mmoja atafuata nyuma.

Wakati kundi hili likifika tayari wachezaji watatu walishawasili ambao ni kipa Diarra Djigui, beki mpya Yannick Bangala na mshambuliaji Yacouba Sogne huku kiungo Khalid Aucho akitarajiwa kuwasili kesho.

Tayari pia makocha wao ukianzia kocha mkuu Nesreddine Nabi na wasaidizi wake wawili pia walishatangulia tangu jana.

Mara baada ya kuwasili Yanga ilipokelewa na wenyeji wao ambao ni maafisa wa klabu ya RS Berkane.

Yanga itakuwa nchini Morocco kwa kambi ya siku zisizopungua 10 wakijiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara na ule wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.