Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 28Article 540313

Habari za michezo of Friday, 28 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga yawaambia Simba, ‘Ohooo! Viporo vinachacha’

Yanga yawaambia Simba, ‘Ohooo! Viporo vinachacha’ Yanga yawaambia Simba, ‘Ohooo! Viporo vinachacha’

TAWI la Simba la Wekundu wa External, limetoa kali ya mwaka baada ya kumuomba Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ kuwapa zawadi watani wao wa jadi Yanga, itakayowasaidia kuunda kikosi bora cha kushiriki michuano ya Caf msimu ujao.

Kama ilivyo ada ya Mwanaspoti kutembelea matawi ya Simba na Yanga, ili kujua shauku yao juu ya klabu hizo, ndipo lilipokutana na kioja cha ombi hilo, huku mashabiki hao kusisitiza bosi wao afanye kama walivyomshauri.

Mjumbe wa tawi hilo, Juma Abdallah Mshuza alisema kutokana na kiwango anachokionyesha straika wao, Chriss Mugalu kuanzia kwenye Ligi Kuu Bara hadi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanaona hastahili kuendelea kubakia Msimbazi badala yake bosi ampeleke tu Yanga.

“Kama kuna maboresho Simba inatakiwa kufanya waongeze washambuliaji wawili wa nguvu, ili Mugalu aende kucheza Yanga ambako ndio saizi yake, hili ombi tunaomba bosi alifanyie kazi na arejee kwenye mechi nyingi ambazo Mugalu amecheza.

“Mastraika kosakosa wapo Jangwani, huku Msimbazi tunahitaji mastraika patapata ambao wataipeleka timu mbele maana tuna kocha mzuri Didier Gomes ambaye anahitaji tumpe ushirikiano wa juu,”alisema Abdallah.

Ukiachana na ushauri wa kumtoa Mugalu zawadi kwa Yanga, shabiki mwingine ambaye ni mwanachama wa tawi hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Waziri Dhahabu alisema kitendo cha timu yao kushindwa kuendelea kwenye michuano ya kimataifa kimeinyima raha Yanga inayojua wazi ubingwa kwao ni ndoto.

“Mimi nacheka tu, wakati mwingine najiulizaga Yanga wana ujasiri gani wa kuona wana nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu wakati wanajua timu yao ni bomu, pia wawe na heshima na Simba imewabeba kimataifa mara ya pili sasa,”alisema Dhahabu.

Tawi hilo lenye wanachama 150 lilianzishwa mwaka jana (2020), ambapo Mwenyekiti wake ni Ramadhan Chambutu na Katibu aliyefahamika kwa jina moja Mark.

Tutumie picha nzuri ya pamoja ya tawi lenu popote mlipo tutaichapisha kwenye ukurasa huu kila Jumatano. Tuma kwa namba 0658 376417

Join our Newsletter