Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 19Article 552490

Soccer News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: Mwanaspoti

Yusuf amtisha Mayele Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Yusuf Athumani Mshambuliaji wa Yanga, Yusuf Athumani

Yanga imesajili washambuliaji watatu tu kuelekea msimu ujao lakini kati yao kuna mmoja tu ndio mzawa na sasa jamaa ameshusha mkwara mzito akisema ujio wake ndani ya timu hiyo sio amekuja kukaa benchi.

Mshambuliaji Yusuf Athuman ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Biashara United ya Mara ameliambia mwanaspoti anajua amekuja kushindania namba na wachezaji wazuri kama Heritier Makambo, Yacouba Sogne na Fiston Mayele lakini anajua atatumia silaha gani kupata namba katika kikosi cha Kocha Nesreddine Nabi.

Yusuf amesema amejipanga kugawana dakika za mchezo kati yake na mastraika hao kazi ambayo ataianza haraka huku huku kambini Morocco kisha atakuja kuendelea nayo, Tanzania.

Usajili wa mshambuliaji huyo Mwanaspoti linafahamu ndio mshambuliaji pekee mzawa aliyependekezwa na kocha Nabi akiwasisitiza mabosi wa Yanga iwe mvua liwe jua kinda huyo lazima avaye jezi za timu hiyo msimu ujao.

“Mimi sijaja Yanga kukaa benchi naijua, nimeichezea nikiwa mdogo na sasa nimerudi tena kufanya kazi hapa siogopi majina nitatumia ubora wangu kufanya zaidi ya kile nilichofanya Biashara mpaka wao wakaniona,” amesema.

“Najua nitapambana juu ya nafasi na wachezaji wa kigeni wenye uwezo nawaheshimu na rekodi zao, lakini mimi kwanza sio mchezaji wa nafasi moja, najua kubadilika kutokana na kila kitu ninacho katika kunisaidia kuonyesha uwezo wangu hapa Yanga muda utaongea.”