Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558292

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Zahera Afunguka Yanga Sc Itakavyowamaliza Wanigeria

Zahera Afunguka Yanga Sc Itakavyowamaliza Wanigeria Zahera Afunguka Yanga Sc Itakavyowamaliza Wanigeria

KOCHA wa zamani wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amemwambia kocha mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi, kuwa kama anataka kufuzu hatua inayofuatia ya Ligi ya Mabingwa Afrika, basi ashambulie kwa dakika zote 90.

Yanga Jumapili hii itajitupa uwanjani huko nchini Nigeria kuvaana na Rivers United katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo hatua ya awali.

Zahera ambaye anasubiriwa kutambulishwa kuwa Mkurugenzi wa Soka la Vijana wa Yanga alisema Yanga ina na nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kama wakifuata maelezo yake.

Aliongeza kuwa, kitu cha kwanza ambacho wanatakiwa kukifanya ni kuwahi kufika Nigeria kwa ajili ya kuandaa mazingira ikiwemo hoteli watakayofikia na uwanja watakaofanyia mazoezi, pia kuhakikisha safu ya ushambuliaji inaongeza umakini kwa kutumia vema kila nafasi watakayoipata.

“Yanga ina uhakika wa kusonga mbele michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani kufungwa nyumbani siyo sababu ya wao kupoteana.

“Uongozi unatakiwa kuwahi kufika Nigeria kwa ajili kuzima hujuma za wapinzani, kwani kujihami ni muhimu na ni ngumu kumuamini mpinzani wako hasa akiwa nyumbani.

“Rivers wataingia uwanjani kwa ajili ya kujilinda zaidi baada ya ushindi ya ugenini, hivyo Yanga wanatakiwa kushambulia kwa tahadhari ya kujilinda.

“Ninaamini kama wakifuata maelekezo hayo, basi Yanga watafuzu kwani hao Rivers siyo wagumu sana, wanafungika vizuri,” alisema Zahera.