Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 25Article 559687

Soccer News of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Zahera ataja Siri ya ushindi Yanga

Zahera ataja Siri ya ushindi Yanga Zahera ataja Siri ya ushindi Yanga

MKURUGENZI wa ufundi Yanga, Mwinyi Zahera amesema siri ya ushindi katika kikosi hicho ni morali ya kutosha kwa wachezaji.

Zahera ambaye alikuwa kocha mkuu katika kikosi hicho amerejea tena hivi karibuni na kupewa cheo Cha ukurugenzi wa ufundi.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba, Zahera amesema;"Umoja wa viongozi na morali kwa wachezaji ndio Siri ya ushindi."

Zahera amesema wachezaji ndio wanastahili pongezi baada ya kufanya vizuri.

Akizungumzia urejeo wake amesema;"Wananchi wajue mimi ni Zahera mpya."