Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572431

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Zidane aonesha dalili kutua Old Trafford.

Zinedine Zidane Zinedine Zidane

Naam, Ole Gunnar Solskjaer bado ni kocha wa Man United. Ipo hivyo mpaka sasa. Zinedine Zidane “Zizzou” anawatizama vigogo wa United kwa mbali….

Ni dhahiri, sehemu kubwa ya mashabiki wa The Red Devils, hawamtaki Ole Gunnar Solskjaer licha ya kuwa, sehemu ya bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo, inampigia chapuo kocha huyo kuendelea kubaki kwenye nafasi yake.

Hali si shwari ndani na nje ya uwanja pale Old Trafford. Mashabiki, baadhi ya wachezaji wa zamani wa United na wachambuzi wa soka, wanasubiri tamko la Solskjaer kuondolewa United. Hakika, tamko linachelewa sana.

Zinedine Zidane ni miongoni mwa makocha wanaohusishwa na Manchester United. Inasemekana kuwa, Zizzou amewaeleza viongozi wa United kuwa, huu sio muda sahihi kwake kutua kwenye EPL. Majira ya kiangazi, ataangalia uwezekano wa kurejea kwenye kazi yake ya ukocha, kwa sasa hapana.

Majibu ya Zidane yanawapa mwanga The Red Devils ambao kwa inavyoonekana, uwezekano wa Ole Gunnar Solskjaer kusalia Old Trafford mpaka mwishoni mwa msimu huu ni mkubwa.