Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573289

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Zidane haiwazii Man United

Zinedine Zidane Zinedine Zidane

Manchester United asubuhi ya Leo Novemmba 21 wamethibitisha kuachana na Meneja wao Ole Gunnar Solskjaer baada ya mfululizo wa matokeo mabovu ndani ya EPL.

Matumaini ya wengi ni kuona kibarua hicho akipewa Zinedine Zidane baada ya makubwa aliyoyafanya akiwa na kikosi cha Real Madrid

Aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane, alishabainisha kuwa kwa sasa yeye anasubiri kupata kazi ya kufundisha timu ya taifa, hatazamii kujiunga na klabu kwa sasa.

Zidane anahusishwa sana na kibarua cha mabingwa Ufaransa, lakini ripoti zinataja kuwa atahitaji kusugua benchi kidogo.

Inatajwa kuwa inawezekana kuwa Zidane tayari ameshakubaliana na dili la kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa lakini anahitaji kusubiri mpaka baada ya Michuano ya Kombe la Dunia huko Qatar mwaka 2022.

Kwa mujibu wa muandishi wa habari, Julien Laurens, Zidane hana mpango wa kwenda Man United au kuonekana kuwa mbioni kuchukua kibarua cha kufundisha klabu kwa sasa.

“Kila mmoja anajuua kuwa baada ya kustaafu Didier Deschamps, ambayo inaweza kuwa baada ya Kombe la Dunia au baada ya Euro 2024, basi kibarua hicho kitakuwa wazi. Na kwa Zidane ni kama wote wameshakubaliana” – Laurens