Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 15Article 542866

Habari za michezo of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Zitto Kabwe ashauri kuwe na wakala wa viwanja vya michezo

Zitto Kabwe ashauri kuwe na wakala wa viwanja vya michezo Zitto Kabwe ashauri kuwe na wakala wa viwanja vya michezo

Siku kadhaa baada ya Serikali kufuta kodi ya nyasi bandia kwenye majiji nchini, mwanasiasa Zitto Kabwe amesema mpango huo unahitaji kuboreshwa.

Zitto amebainisha hayo leo Jumanne katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital yaliyofanyika makao makuu ya Kmapuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Amesema kitendo cha Serikali kuondoa kodi ya nyasi bandia ni jambo jema na la maandeleo katika michezo nchini, lakini ungeboreshwa na kufanyika nchi nzima.

"Viwanja vingi nchini ni vibovu na vingi vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambavyo vingi imeshindwa kuviboresha.

"Ingekuwa vema kama vingerudishwa kwa Serikali au tukaanzisha wakala wa viwanja vya michezo ambaye atasimamia viwanja nchini kuhakikisha vinakuwa bora," amesema.

Amesema pia mkakati wa Serikali kuondoa kodi kwenye nyasi bandia ni mkakati mzuri, lakini wanafaika kwenye mpango huo ni wachache.

"Watakaoondolewa tozo hiyo ni majiji ya Tanga, Arusha, Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

"Kwa kuipa unafuu majiji kwenye hilo kunaweza pia kuleta urasimu, mtu akaagiza nyasi kumbe anazipeleka Tabora lakini akadanganya anazipeleka Dodoma.

"Hivyo ingekuwa bora mpango huu wa nyasi bandia ungeilenga mikoa yote nchini," amesema Zitto.