Uko hapa: NyumbaniMichezoRiadha2021 11 15Article 571396

Track & Field News of Monday, 15 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hamilton bingwa Sao Paulo Grand Prix

Lewis Hamilton Lewis Hamilton

Mwanalanga langa mashuhuri, Lewis Hamilton amefanikiwa kutwaa ubingwa wa mbio za Sao Paulo GP baada ya kumpiku mpinzania wake Max Verstappen.

Hamilton aliongoza raundi kumi na mbili akitokea nafasi ya kumi na kupambana na Verstappen na kutwaa ubingwa kwa utofauti wa alama 14.

Huu unakuwa ni ubingwa wa 101 kwa Hamilton akituma ujumbe muhimu wa ubabe wake katika mbio hizo za langalanga duniani.

Endapo Verstapen angeweza kumzuia Hamilton, angeweza kumalika katika nafasi ya pili nyuma ya dereva wa Mercedes zikiwa zimebaki mbio tatu, Qatar, Saudi Arabia na Abu Dhabi na kushinda taji.

Baada ya mbio hizo za Sao Paulo GP, Lewis alipigwa faini ya Euro 25,000, wakati Euro 20,000 zimezuiwa mpaka mwisho wa msimu wa 2022, iliyohusishwa na kuvunja sheria za kutofunga mkanda wakati wa mzunguko wa majaribio.