Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 09 29Article 560368

Muziki of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Albamu ya Ali Kiba Octoba 7

Cover ya Albamu ya Ali Kiba Cover ya Albamu ya Ali Kiba

Hatimaye msanii wa muziki wa Bongofleva nchini Tanzania Alikiba, ametaja siku anayotarajia kuachia albamu yake mpya ambayo ni Oktoba 7.

Kiba ametangaza ujio wa albamu hiyo leo Jumatano Septemba 29,2021 Jijini Dar es Salaam, ambapo pia aliitambulisha kwa jina kuwa itaitwa ‘Only One King’.

Ujio huo wa albamu, Alikiba alianza kuutangaza tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini hakuweka wazi kuwa ni lini haswa ataiachia.

Badala yake alikuwa akiachia nyimbo moja moja tangu mwaka umeanza na mpaka sasa ana nyimbo zisipungua nne huku zote zikiwa zinafanya vizuri.

Hii itakuwa albamu ya tatu kwa msanii huyo ikitanguliwa na ‘Cinderela’ iliyotoka mwaka 2007 na kufuatiwa na ile ya ‘Ali K 4real’ aliyoitoa mwaka 2009.

Katika nyimbo alizoachia ipo ya Jelous aliyoimba na msanii Mayorkun kutoka nchini Nigeria, ambayo ndio inaongoza katika nyimbo zake alizotoa mwaka huu kutazamwa mara nyingi youtube kwa kuwa na watazamaji milioni saba.

Ipo pia nyimbo ya ‘Salute’ aliyomshirikisha Rudeboy naye msanii kutoka nchini Nigeria ambaye zamani walikuwa wanaunda kundi la P.Square.

Nyingine ni wimbo wa ‘Ndombolo’ alioimba kwa kuwashirikisha wasanii wa lebo yake ya Kings music akiwemo mdogo wake Abdukiba, K2GA na Tom Flavour. Wimbo wa nne ni wa Infidele, alioachia Januari mwaka huu.