Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 09 09Article 556375

Muziki of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: millardayo.com

BSS Msimu Mpya: Salama afunguka kuhusu mshindi anayemtaka

Salama Jabir atambulishwa kama Jaji BSS play videoSalama Jabir atambulishwa kama Jaji BSS

Baada ya usiku wa jana kuzinduliwa kwa mashindano maarufu ya kusaka vipaji ya Bongo Star Search (BSS) kwa msimu wa 12, salama Jabir pia alikua ni miongoni mwa watu waliotambulishwa kama mmoja watakaokwenda kuwa majaji wa mashindano hayo kwa mwaka 2021.

Salama alishawahi kuwa jaji wa mashindano hayo hapo kabla laikini akapotea kwa takribani misimu miwili.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.

Baada ya utambulisho huo salama amezungumza vitu mbali mbali kuelekea katika mashindano hayo kwa mwaka 2021.