Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 03 17Article 528709

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 17 March 2021

Chanzo: zanzibar24.co.tz

MACZA YAJA NA MACZA STAA FESTIVAL

Tasisi ya Matofali Arts Creation (MACZA) inatarajia kufanya Tamasha la Wasanii linaloitwa  MACZA STAA FESTIVAL ambalo litawashikirisha wasanii kutoka   Unguja na Pemba linalotarajiwa kuanza  tarehe 21 ya mwezi huu na kumalizika tarehe 28.

Akizugumza na Waandishi wa Habari huko katika Ukumbi wa Sanaa uliopo Rahaleo Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Matofali Mohamed Said Mwinchande amesema Tamasha hilo lina lengo la kuinua vipaji vya wasanii kutoka sehemu tofauti ndani ya Zanzibar.

Amesema taasisi hiyo ina dhamira ya kuifanya Sanaa ya Zanzibar kuwa ni sehemu ya ajira kama zilivyo ajira nyengine ili waweze kujikimu kimaisha na kujiongezea kipato kupitia Sanaa .

Amesema tamasha hilo linatarajiwa kuadhimishwa kwa shughuli mbali mbali za kazi za sanaa na utamaduni na inalenga kumtangaza staa aliobobea katika tasnia ya Sanaa ya maigizo.

Aidha amesema kuanzishwa kwa Tamasha hilo kutawasaidia Wasanii kufikia ndoto zao na kukuza vipaji vya Wasanii wa filamu, maigizo na ngoma za kiasili Unguja na Pemba ambalo litakuwa linafanyika kila mwaka Nchini.

Pia amesema matarajio ya taasisi hiyo ni kuonesha kazi na shughuli mbali mbali za wasanii kujenga uwezo na kuwa na kiwanda cha kukuza ubunifu na kuzalisha kazi zinazokubalika kwa jamii na kimataifa.

Hata hivyo ameema tamasha hilo litafunguliwa kwa kufanya shughuli za usafi wa mazingira katika fukwe za Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mgeni Rasmi.

Vile vile litaendelea tarehe 26 ya mwezi huu Wasanii watafafanya matembezi yatakayoanzia Magogoni kwa Mabata,Mwanakwerekwe, Magomeni, Kidonge chekundu , kuteremkia Bomani , Miembeni na kumalizia Mapinduzi Square.

Na tarehe 28 ndio itakuwa siku ya maadhimisho ambayo shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Iddriss Abdulwakil kwa sherehe mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumvalisha taji Staa kutoka Sanaa ya maigizo Zanzibar.

Tamasha hilo linatarajiwa kuadhimishwa kwamuda wa  siku nne katika tarehe mbali mbali  linalotarajiwa kuanzia tarehe 21-28 ya mwezi huu ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni MSHIKAMANO NA EIMU KWA WASANII NDIO NJIA PEKEE YA KULETA MABADILIKO NA MAENDELEO YA SANAA NCHINI.

Story na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.

Join our Newsletter