Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 10 12Article 562717

Muziki of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mauzo ya R. Kelly yaongezeka

Mwanamuziki nguli R. Kelly Mwanamuziki nguli R. Kelly

Mauzo ya muziki wa Msanii Robert Kelly (R. Kelly) yameongezaka kwa zaidi ya asilimia 500 tangu staa huyo wa R&B alipokutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake.

Kwa mujibu wa jarida la Rolling Stone, mauzo ya kazi za R. Kelly mwenye umri wa miaka 54 yamepanda kwa asilimia 517.

Msanii huyo mzaliwa wa Chicago, alikutwa na hatia Septemba 24, mwaka huu, na kama si miaka miaka 10 gerezani, basi atahukumiwa kifungo cha maisha.

Mauzo ya album ya R. Kelly yameongezeka kwa 517%, huku usikilizaji mitandaoni ukifikia milioni 13.4 kutoka milioni 11.2, tangu alipotiwa hatiani kwa makosa mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kingono.

Hivi karibuni YouTube ilifungia akaunti zake mbili kwa kukiuka sera za mtandao huo.

Mei 4, mwakani, ndiyo siku ya hukumu yake na ndipo atakapoangukiwa na moja kati ya adhabu hizo.