Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 08 20Article 552769

Muziki of Friday, 20 August 2021

Chanzo: Bongo5

Mr Blue kafikisha kolabo 1000, akataa kuitwa legendary

Mwanamuziki wa Bongo Flavour play videoMwanamuziki wa Bongo Flavour

Msanii wa muziki wa Bongo Flavour, Heri Samir "Mr blue" Ijumaa hii amezungumza na waandishi wa habari wakati akim-support msanii mpya wa Singeli, Elisha kutoka lebo ya boss kapaka Entertainment ambapo rapa huyo alipata kufunguka mengi kuhusu muziki wa BongoFleva.

Rapa huyo amesema yeye ni msanii ambaye amefanya kolabo nyingi zaidi ambapo amedai mpaka sasa amefanya zaidi ya kolabo 1000 za wasanii tofauti tofauti, wakubwa kwa wadogo.

Amesema amekuwa akifanya hivyo ili kuibua na kuwapa nafasi wasanii wapya wenye vipaji huku akimtolea mfano msanii wa Singeli dogo elisha ambaye ameachia naye kolabo ya pamoja ya wimbo, Unanikosha remix.