Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 08 17Article 551959

Muziki of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Penzi letu sio la kwanza kuisha" - Billnass kuhusu Nandy

Nandy na Billnas Nandy na Billnas

Baada ya tetesi kuwa nyingi zinazohusu kuachana kati ya rapa Billnas na mlimbwende kunako game ya Bongo flavour Nandy, Sasa Kupitia page ya Instagram anayotumia rapa Billnass siku za hivi karibuni ameshea picha mbili na video moja akiwa amemshika mtoto ambaye amem-tag kwa jina la Nenga Tronix, huku wakisindikizwa na ujumbe unaosomeka "LA FAMILIA".

Watu wengi wameuliza kuhusu mtoto huyo na  wengine wakitaka kujua mama wa mtoto huyo, na vipi hatma yake na Nandy ambao stori zinasemekana wametemana kwa sasa.

Sasa leo kupitia Insta story yake amezua gumzo kwa kupost ujumbe unaotafsirika kama hali si shwari kwenye mahusiano yake na Nandy baada ya kuandika.

"Penzi letu sisi sio la kwanza kuisha, ugomvi wetu yeye hajui chanzo wala kisa yeye ni malaika usimuweke kwenye vita" 

Wawili hao yalijulikana wazi kuanzia mwaka 2018 na miaka miwili baadaye 2020 walichumbiana na kuvishana pete katika moja ya vipindi vya "Live" vinavyorushwa na moja ya kituo cha televisheni hapa nchini, na kuahidiana mipango ya ndoa.