Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 08 13Article 551293

Muziki of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

VIDEO MPYA: AY karudi na "Stakaba"

Wasanii wa bongo fleva, AY (kushoto) na mwana Fa play videoWasanii wa bongo fleva, AY (kushoto) na mwana Fa

Msanii wa bongofleva na anayefanya vyema kunako game hiyo, Ambwene Yesaya (AY) hii leo Agosti 12, ameachia ngoma mpya baada ya ukimya wa kipindi cha takriban miezi kadhaa.

Katika ngoma hiyo inayojulikana kama "Stakaba", AY amemshirikisha "Chuga Queen" MIMI Mars wakati akiitambulisha kwa mara ya kwanza katika kituo cha Redio, Clouds Fm mchana wa leo.

AY ambae aliongozana na swahiba wake wa muda mrefu, Msanii na Mbunge wa Muheza Hamis Mwin'juma (Mwana Fa), imetengenezwa na Producer Daxo Chali kutoka studio za Mj Records.

Ngoma hiyo pia imeachiwa na Video ambayo imetengenezwa na Slide digital huku ikisimamiwa na Mx Carter na Freeman Richard kama Ma-director.

AY ameshatamba na nyimbo nyingi Kitaifa na Kimataifa kama vile Freeze aliowashirikisha P square,zigo,Party zone na nyingine nyingi.