Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 08 16Article 551764

Muziki of Monday, 16 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri atoa neno kufungia kazi za wasanii

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Innocent Bashungwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Innocent Bashungwa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amefunguka kwamba jukumu la Serikali ni kukuza sanaa kwa kuwa ni sehemu muhimu sana ambayo inatoa fursa za ajira na kukuza kipato kwa wananchi lakini katika kukuza sanaa ni lazima wasimamie mila, desturi na maadili.

Waziri Bashungwa amesema hayo katika mahojiano yake na kipindi cha DADAZ, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha East Africa Televisheni leo Agosti 16,2021.

Bashungwa amesema kwa nia njema ya kukuza sanaa ni lazima wasimamie mila, desturi na maadili ya nchi na hakuna Taifa ambalo halina utambulisho wa mila na desturi.

Aidha, amesema kuhusu suala la maadili na kufungiwa kwa wasanii hawataweza kukubali kwa sababu ya kutaka kukuza sanaa na kutengeneza ajira, na wataendelea kusimamia Sheria kwa wasiofuata taratibu hivyo wakati wanakuza sekta ya Sanaa wao kama Serikali watahakikisha na suala la mila, desturi na maadili vinakwenda sambamba.

Vile vile Bashungwa amesema wapo kwenye kupitia kanuni ambazo kimtazamo zinaonekana ni za kizamani lakini ili kuondokana na sintofahamu wanashirikisha wadau na watakuja na muongozo maalum.