Uko hapa: NyumbaniBurudaniMuziki2021 09 01Article 554797

Muziki of Wednesday, 1 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Whozu afanya Wimbo kuelekea Siku ya "Simba day"

Msanii wa Bongo Flavour, Whozu play videoMsanii wa Bongo Flavour, Whozu

Klabu ya Simba leo Septemba 1, Kupitia kwa Kaimu Afisa habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amezungumza na Waandishi wa habari kuwafahamisha kuhusiana na suala la Jezi za msimu mpya 2021/22 na mipango kuelekea tamasha la "Simba day"

Miongozi mwa watu waliozungumza ni Msanii whozu ambae amefanya wimbo wenye ladha tofauti kama zawadi kwa ajili ya mashabiki wa Simba SC.

“Nimetengeneza wimbo utakuwa maalumu kwaajili ya mashabiki wa Simba SC nimefanya hivyo kutokana na mapenzi ya timu yangu ya Simba SC, nimefanya hivyo kutokana na Ubingwa wa timu yangu”-

“Kwahiyo ni faraja kufanya kitu kizuri au kutengeneza ama kufanya ubunifu ni ushindi pekee kinajitangaza, asilimia kubwa ya baadhi ya nyimbo za wenzetu uwa wanawekeza kwenye nyimbo za Singeli lakini kwa upande wangu nimechanganya vitu tofauti tofauti kidogo nimeweka Bolingo, Singeli,Bongo Fleva sikutaka kukaa kwenye upande mmoja”– amesema Whozu