Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 09 09Article 556501

Mpira wa Kikapu of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Ben Simmons awaduwaza 76ers

Ben Simmons awaduwaza 76ers Ben Simmons awaduwaza 76ers

Mchezaji wa kikapu kutoka nchini Australia Ben Simmons ameweka wazi kwa ataondoka katika timu ya Philadephia 76ers ambayo inashiriki Ligi ya kikapu nchini Marekani maarafu kama NBA.

Simmons amegoma kurudi katika kambi ya timu hiyo iliyoanza mwezi septemba 28, na kufanya mambo yazidi kuwa magumu kwa timu yake ambayo inapata kigugumizi cha kumuuza mchezaji huyo mkubwa ambaye thamani yake imeshuka.

76ers, wanapata ugumu huo kutokana na uhitaji wa wachezaji wenye kiwango cha juu kupitia mauzo ya Simmons kutoka kwenye timu ambayo itahitaji huduma yake lakini kutokana na kushuka kwa thamani ya mchezaji huyo watalazimika kupata wachezaji wa daraja la kati.

Ujumbe ambao Simmons ametuma kwa Uongozi wa timu yake ni kwamba sio kazi yake kupandisha thamani ya biashara ya mauzo na hicho sio mkakati wake kwasasa.