Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 08 13Article 551374

Mpira wa Kikapu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Kawhi Leonard afanya maamuzi mazito LA Clippers

Kawhi Leonard, Mchezaji wa Mpira wa Kikapu Kawhi Leonard, Mchezaji wa Mpira wa Kikapu

Mcheza kikapu wa timu ya Los Angeles Clippers ya NBA, Kawhi Leonard amesaini kandarasi ya miaka minne kuendelea kusalia Clippers hadi mwaka 2026, mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 178 sawa na bilioni 412 na zaidi ya milioni 782 za kitanzania na kumfanya kuingia kwenye oro

Kawhi alisaini kandarasi hiyo usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2021 baada ya kuwa mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na wakali hao wa jiji  la Los Angeles lakini, Rais wa timu hiyo Lawrence Frank alisema wamemuongezea kandarasi hiyo Kawhi kwasababau ni mchezaji ambaye anakua na ana mahusiano mazuri na ya muda mrefu na klabu.

Frank amesema. “Kawhi ni mchezaji ambaye anakuwa kila siku, malengo yetu mengi yanafanana pamoja na kuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu na timu. Tumemsajili kumtaka awepo anapopenda kuwepo na wachezaji wenzake”.

Frank pia amewatoa shaka juu ya matibabu ya Kawhi na kusema kwa sasa wanafanya na watafanya lolote liwezekanalo kumuunga mkono Leonaed kweny e klinic yake anayoendelea kutpata matibabu.

Kawhi alijiunga na Clippers miaka miwili iliyopita akitokea timu ya mabingwa wa NBA wa msimu juzi, Toronto Raptors na kuunga na Paul George ili kuunda project nyingine ya kutaka kushinda NBA baada ya kufanya hivyo na Raptors.

Na mkataba huo umekuja baada ya kuzidi kuonesha kiwango safi cha kuwa na wastani wa alama 26, rebounds 7 na assist 5 kwa msimu ulioisha.