Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 10 06Article 561724

Mpira wa Kikapu of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Kengele ya moto yahairisha mchezo NBA Pre-season

Brooks Lopez wa Milwaukee bucks (katikati) akiwania mpira na walinzi wa Memphis Glizzlies, Brooks Lopez wa Milwaukee bucks (katikati) akiwania mpira na walinzi wa Memphis Glizzlies,

Mchezo wa kirafiki wa maandalizi kuelekea msimu ujao wa NBA mwaka 2021-22 kati ya Memphis Glizzlies na Milwaukee Bucks umeahirishwa baada ya kengele ya kuashiria moto umewaka kulia baada ya kuguswa na mtu asiyejulikana.

Wakati kengele hiyo inalia Memphis ilikuwa inaongoza kwa alama 87-77 kwenye robo ya tatu jambo lililopelekea mchezo huo kusimama na watu wa usalama kuanza kuwatoa nje watazamaji waliokuwepo kwenye dimba la FedEXForum.

Baada ya sekeseke hilo, watu wa usalama walitoa ufafanuzi kwa kusema hakukuwa na moto.

NBA ikatoa tamko la kuhairishwa kwa mchezo huo baada ya zaidi ya dakika 60 kupita na sababu ya pili wakieleza kulinda usalama zaidi wa wachezaji.

Michezo mingine NBA Pre-season iliyochezwa alfajiri ya kuamkia leo ni New York Knicks iliyopata ushindi wa alama 125-104 Indiana Pacers, Houston Rockets 125-119 Washington Wizard wakati Chicago Bulls 131-95 Clevelanda Cavaliers.

Michezo ya Pre-season itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 7, Phoenix Suns itacheza na LA Lakers saa 7:00 usiku, Detroit Pistons dhidi ya San Antonio Spurs saa 8:00 usiku wakati New Orlean Pelicans itakipiga na Orlando Magic saa 9:00 usiku.

Utah Jazz watakuwa ugenini kwa Dallas Mavericks saa 9:30 usiku, Golden State Warriors watacheza na Denver Nuggets saa 11:00 Alfajiri ilhali Los Angeles Clippers itachuana na Sacramento Kings saa 9:30 usiku wa kuamkia kesho Oktoba 7, 2021.