Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 05 25Article 539794

xxxxxxxxxxx of Tuesday, 25 May 2021

Chanzo: eatv.tv

Lakers kujiuliza kwa Phoenix Suns NBA Playoff

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya kikapu nchini Marekani 'NBA', timu ya Los Angeles Lakers imeibua hofu ya kutetea taji hilo baada ya kukubali kufungwa usiku wa kuamkia leo na Phoenix Suns kwa alama 99 kwa 90 ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kwenye NBA Playoff.

Submitted by George David on Jumanne , 25th Mei , 2021 Nyota wa Phoenix Suns, DeAndre Anthony akijaribu kufunga mbele ya walinzi wa LA Lakers kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa wikiendi iliyipita.

Lakers wanauhitaji wa kushinda michezo yake minne kati ya mitano iliyosalia kwenye hatua hiyo ya mtoano ili kutinga hatua ya nusu fainali ya NBA kwa upande wa Mashariki mwa ligi hiyo ambayo mpaka hivi sasa vinara wa upande huo Philadelphia 76ers wakionekana kufanya vizuri.

Michezo ya mtoano ya NBA itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo mitatu huku Lakers wakishuka tena na Phoenix Suns saa kumi na moja Alfajiri, Brooklyn Nets itakipiga tena na Boston Celtics saa nane na nusu usiku huku Nets ikiwa inaongoza kwenye michezo  yote miwili.

Kwa upande mwingine, Los Angeles Clippers watajiuliza kwa Dallas Mavericks baada ya kukubali kichapo kwenye mchezo uliopita, mchezo utakaochezwa saa kumi na moja alfajiri ya kuamkia kesho kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Join our Newsletter