Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2022 01 13Article 585538

Mpira wa Kikapu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Lakers yadunda kwa Sacramento, Harden akiinyanyua Nets

LA Lakers wapoteza kwa mara nyingine NBA LA Lakers wapoteza kwa mara nyingine NBA

Los Angelea Lakers wamepoteza mchezo wao wa 21 leo kwa kukubali kipigo cha points 125-116 kutoka kwa Sacramento Kings.

De’Aaron Fox aliiongoza vyema Sacramento kwa kufunga points 29, rebounds 4 na assists 4 katika ushindi huo wa 17 kwa Sacramento msimu huu huku wakiwa wameshapoteza michezo 27.

James Harden amefunga mitupio 5 ya points 3, akifunga jumla points 25, rebounds 7 na assists 16 kuiwezesha Brooklyn Nets kupata ushindi wake wa 27 msimu huu huku wakiwa wamepoteza michezo 14.

Baada ya kushinda dhidi ya Sacramento Kings Jumatatu, Cleveland Cavaliers wameendeleza ushindi wao kwa kuwapiga Uttah Jazz kwa vikapu 111 kwa 91.

Huu unakua ushindi wa 24 kwa Cavs huku wakiwa wamepoteza michezo 18 mpaka sasa msimu huu.

Boston Celtics wakiwa nyumbani wamewafunga Indiana Pacers kwa jumla ya vikapu 119 kwa 100.

Jayson Tatum alikua na wakati mzuri leo akifunga points 33, rebounds 7, kutoa assists 4 huku akizuia mipira mara 2.

Matokeo mengine ni kama inavyoonekana kwenye jedwali.