Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 11 25Article 574069

Mpira wa Kikapu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

LeBron Arejea na Ushindi Lakers

Nyota wa  Los Angeles Lakers , Le bron James Nyota wa Los Angeles Lakers , Le bron James

Baada ya kufungiwa mchezo mmoja, LeBron James amerejea uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Indiana Pacers kunako NBA.

James alifungiwa kucheza mchezo mmoja baada ya kuhusika kwenye ugomvi na Isaiah Stewart wikiendi iliyopita.

Japokuwa Lakers wameshinda kwa pointi 124-116, kwa sehemu kubwa walikuwa wametawaliwa na Pacers mchezoni. James alipachika jumla ya pointi 39 huku Russell Westbrook akiongeza pointi zingine 20.

Kwingineko kwenye NBA;

Suns wameshinda kwa pointi 120-115 dhidi ya Cavaliers, Warriors wameshinda 116-96 dhidi ya 76ers, Nets wameshinda 114-93 dhidi ya Pistons na Rockets wamepindua meza kwa kushinda 118-113 dhidi ya Bulls.