Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Kikapu2021 10 13Article 562981

Mpira wa Kikapu of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Sean: Kyrie Irving hatocheza Brookly Nets NBA

Nyota wa Brooklyn Nets, Kyrie Irving. Nyota wa Brooklyn Nets, Kyrie Irving.

Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Brooklyn Nets, Sean Marks amesema hali ilivyo kwasasa mchezaji wao nyota Kyrie Irving hatoweza kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake na hata kuhusishwa kwenye masuala ya timu kwasababu bado hajapata chanjo ya Covid-19.

Sean amesema, “Kwasasa uamuzi wake una mzuia kuwa na timu katika mazingira yote. Na hatutomruhusu mtu yeyote wa timu yetu kushiriki nusu nusu. Kulingana na hali ilivyo, Kyrie Irving hatocheza wala kufanya mazoezi na timu mpaka atakapokuwa mchezaji halali kuruhusiwa kucheza”.

Msimamo huo wa Brooklyn umekuja baada ya sheria na taratibu za mji wa New York kusomeka kuwa, wachezaji na watu mashuhuri wengine ni lazima wachanje ili wahusike kwenye mikusanyiko na hata kwenye michezo yao ya ligi mbali mbali ikiwemo Covid-19.

Ikumbukwe kuwa Irving aliweka wazi msimamo wake juu y chanjo ya Covid-19 na kusema, “Mimi ninalindwa na Mungu, pamoja na watu. Tunasimama pamoja”.

Tyari Kyrie amekosa michezo mitatu ya NBA Pre-season ukiwemo ushindi wa kibabe mbele ya wapinzani wao Los Angeles Laker.