Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 09 06Article 555499

Boxing News of Monday, 6 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Bondia Mwakinyo Apanda Ubora Duniani

Bondia Mwakinyo Apanda Ubora Duniani Bondia Mwakinyo Apanda Ubora Duniani

BONDIA Mtanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.

Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter. Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.

Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24. Na Nimeendelea kuwa Bingwa wa ABU na Bondia namba 1 Africa,’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hassan Mwakinyo alijitosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.