Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 11 21Article 573121

Boxing News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Cheka, Alkasusu mbabe kujulikana Desemba 3

Cheka, Alkasusu mbabe kujulikana Desemba 3 Cheka, Alkasusu mbabe kujulikana Desemba 3

MABONDIA wa ngumi za kulipwa Cosmas Cheka na Muhsini Swalehe ‘Alkasusu’ wametambiana mbele ya waandishi wa habari kuhusu pambano linalotarajiwa kuchezwa Desemba 3 Uwanja wa Kinesi, Urafi ki, Dar es Salaam.

Wakizungumza jana Alkasusu alimuonya Cosmas Cheka kuwa kama anategemea kuvaa ‘hogo’ siku ya pambano lao na yeye atavaa halafu watapigana kwa mkono mmoja kwani mashabiki wa ngumi wamechoka na maigizo yake ya Bongo movie.

“Cosmas nakuambia mbele ya waandishi wa habari siku ya pamabano usije kujifanya umeumia mkono maana na mimi nitafunga mkono halafu tupigane ngumi kwa mkono mmoja. Kwanza wewe unabebwa na umaarufu wa kaka yako Francis Cheka,” alisema Alkasusu.

Naye Cosmas alikanusha kubebwa na umaarufu wa kaka yake na kusema yeye amepigana mapambano mengi ya kitaifa na kimataifa na ulingoni anapanda peke yake wala siyo kaka yake. “Mimi nimepigana ndani nanje na ulingoni napanda peke yangu bila kaka yangu hivyo unavyosema umaarufu wake ndio unanibeba unakosea ila maneno yako ni sawa na unavyotembeza Alkasusu mtaani hivyo siku hiyo nitakuonesha ngumi zinavyopigwa,” alisema Cosmas.

Naye mwaandaji wa pambano hilo kampuni ya Grobox Sports Promotion, chini ya promota Sia Mosha alisema wamezindua kampuni hiyo ambayo itakakuwa ikifanya matukio mbalimbali ya burudani lakini wameanza na mchezo wa ngumi kwa kuwakutanisha wababe hao kwenye ulingo ili kuoneshana ubavu.

“Kitu cha kwanza tumezindua na kuitangaza kampuni yetu ya Grobox Sports Promotion ambayo itakuwa ikijihusisha na masuala ya burudani lakini kwa sasa tumeanza na mchezo wa ngumi ambao umekua, tumeandaa pambano ambalo litawakutanisha Alkasusu na Cosmas Cheka kama pambano kuu.