Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 11 22Article 573457

Boxing News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Crawford amstaafisha ndondi Shawn Porter

Shawn Porter akiwa ameanguka baada ya kupokea konde zito Shawn Porter akiwa ameanguka baada ya kupokea konde zito

Terence Crawford alimpiga kwa TKO bondia Shawn Porter katika raundi ya 10 siku ya Jumamosi usiku na ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Porter kupokea kichapo cha Knockout na alibainisha kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho wakati akifanya mahojiano ya waandishi baada ya pambano kumalizika.

Porter mwenye umri wa miaka 33 alitangaza kwamba amestaafu mchezo huo na angefanya hivyo hata kama ingetokea yeye ameshinda pambano hilo hata kama wangeenda sare mipango yake ilikuwa ni kuachana na mchezo huo unapendwa ulimwenguni.

“Nilijiandaa kutangaza kustaafu ndondi leo usiku iwe kushinda, kupoteza au droo,” Porter aliongea kwenye mkutano ambao ulihudhuriwa na vyanzo mbalimbali vya habari. “Sitaendelea kucheza tena natangaza kustaafu hivi sasa.

“Baada ya kupigana na kila bondia aliye kwenye kiwango cha juu nini cha zaidi naweza kufanya? Siendi kuwa mlinzi hayo siyo maisha ninayotaka kuishi sitaki kuwa bondia ambaye nitagombana hata wakati nikiwa na umri wa miaka 40 huko,”

Porter amepigana na mabondia kama Crawford, Errol Spence Jr, Keith Thurman, Yordenis Ugas, Danny Garcia na Adrien Broner na amepoteza kwa Crawford, Spence, Thurman na Kell Brook na aliwapiga Garcia, Ugas na Broner.