Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 06 12Article 542377

Boxing News of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dulla Mbabe: Kiduku hanipigi tena

Dulla Mbabe: Kiduku hanipigi tena Dulla Mbabe: Kiduku hanipigi tena

BONDIA Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema anatarajiwa kuanza maandalizi ya kujifua kuanzia Jumatatu ijayo kulipiza kisasi dhidi ya mpinzani wake mkubwa Twaha Kiduku.

Mabondia hao wanatarajiwa kupanda ulingoni Julai 24, mwaka huu kuchuana katika pambano la mizunguko 10 lisilokuwa la ubingwa.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam hivi karibuni Dulla Mbabe alisema anaamini kwa maandalizi mazuri atakayofanya atahakikisha hapigwi tena.

“Natarajia kuanza maandalizi kuanzia Jumatatu, nataka kujiweka vizuri nikiamini nitakayekutana naye sio mtu wa kumdharau. Mara ya mwisho alinipiga ila sasa sitaki yajirudie tena,”alisema.

Pambano la mwisho walikutana Agosti mwaka jana ambapo Kiduku mwenye makazi yake Morogoro alishinda.

Dulla Mbabe alisema awamu hii lazima mpinzani wake huyo aangukie pua kwani hatokubali kushindwa kiurahisi.

Alisema licha ya kwamba bondia huyo ni mzuri mwenye uwezo atakabiliana naye kwa kuwa tayari anajua mbinu zake kuhakikisha anamaliza ubishi kwa mashabiki kuwa hamuwezi.

Mwezi uliopita bondia huyo anayeshika nafasi ya pili nchini katika uzito wa super middle, alipoteza pambano la kimataifa dhidi ya Mrusi Pavel Silyagin lililofanyika Urusi.

Habari

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni