Uko hapa: NyumbaniMichezoNdondi2021 05 27Article 540226

Boxing News of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mwakinyo aahidi kumpiga Muangola kama zawadi kwa Rais Samia

Mwakinyo aahidi kumpiga Muangola kama zawadi kwa Rais Samia Mwakinyo aahidi kumpiga Muangola kama zawadi kwa Rais Samia

Mwakinyo ambaye atawania mkanda wa Afrika (ABU) wa uzito wa Super welter atapanda ulingoni kesho kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports.

Amesema kuwa amejiandaa vyema na kwa vile atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wa Rais Samia, hatofanya makosa zaidi ya kushinda katika raundi za mwanzoni tu katika pambano hilo lililodhaminiwa na KCB Bank, Plus TV, Multichoice Tanzania, Tanzania Tourism Board, Onomo Hotel, Precision Air, Prestine Logistics, Urban Soul na washirika wa kimataifa Global Boxing Stars na Epic Sports Entertainment.

“Nitakuwa napigana kwa mara ya kwanza chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan, sitamwangusha Rais na watanzania kwa ujumla, nawaomba mashabiki kufika kwa wingi ili kunipa sapoti,” amesema Mwakinyo.

Wakati Mwakinyo anasema haya, mpinzani wake Mayala amesema kuwa pamoja na kupata taarifa za muda mfupi, amejiandaa vyema ili kuonyesha kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa.

“Nimekuja kwa ajili ya kushinda na si kupoteza, nilikuwa nafanya mazoezi kwa sababu ngumi ni kazi yangu na siwezi kuruhusu Mwakinyo kushinda na kuchukua mkanda wa Afrika,” amesema Mayala.